Hapa na Pale
KM ameripotiwa kukaribisha hatua iliochukuliwa ya kupitisha Mwito wa a Viongozi wa Taifa na Serikali wa Eneo la Maziwa Makuu juu ya Mpango wa Amani wa Burundi, kwenye Mkutano uliofanyika Bujumbura mnamo Disema 04 2008, ambao uliandaliwa na Raisi Yoweri Museveni wa Uganda. KM aliinasihi Serekali ya Burundi pamoja na kundi la Palipehutu-FNL kujitahidi tekeleza, kwa ukamilifu, na kwa imani kuu, mapatano yao yaliofikiwa kenye mkutano wa Bujumbura ili kuhakikisha amani itadumishwa nchini.
Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limeeleza kwamba limo mbioni kukamilisha maafikiano ya kusitisha mapigano miongoni wa makundi yanayohasimiana Kivu Kaskazini. Juhudi hizi zinaashiriwa zitafufua, kwa nguvu zaidi, mazungumzo ya amani. Kadhalika imeripotiwa vikosi ziada vya MONUC vinaendelea kuenezwa katika Kivu Kaskazini, ambapo karibuni pia vikosi vya amani vya UM veyenye kuzungumza Kifaransa vilipelekwa Goma, halkadhalika, kuimarisha zaidi ulinzi wa raia. Helikopta za MONUC zipo tayari kuendeleza operesheni za dharura pindi raia watahujumiwa. Vile vile vikosi maalumu vya UM hivi vimesambazwa kulinda maeneo ya hatari mipakani kati ya JKK na Rwanda.