Darzeni za mataifa yamechangia kutia sahihi Oslo mkataba wa kupiga marufuku mabomu ya mtawanyo

Darzeni za mataifa yamechangia kutia sahihi Oslo mkataba wa kupiga marufuku mabomu ya mtawanyo

Kuanzia tarehe 02 mpaka 04 Disemba, wawakilishi wa kutoka nchi 100 ziada walikusanyika kwenye mji wa Oslo, Norway kutia sahihi mkataba uliodhaminiwa na UM, wenye kuzitaka nchi wanachama zote kuahidi kuwacha kutengeneza, kutumia au kurimbikiza na kuhamisha zile silaha za mabomu ya mtawanyo, yaani zile silaha ambazo mara nyingi huua raia wasio hatia, na kulemaza jamii mbalimbali za umma wa kimataifa, muda mrefu baada ya uhasama kusitishwa. ~~

Silaha za klasta zilitumiwa, kwa mara ya kwanza kimataifa, katika Vita Kuu ya Pili. Kila bomo moja la klasta linakadiriwa hubeba darzeni za vijibomu vidogo vidogo, ambavyo baada ya kufyatuliwa kutoka makombora, hutawanyika na kusambaa kwenye sehemu kubwa ya ardhi, eneo ambalo ukubwa wake ni sawa na viwanja viwili-vitatu vya mpira. Vijibomu hivi mara nyingi hukwama ardhini baada ya kufyatuliwa, na hujizatiti chini ya kwa muda mrefu, vikingokea kudhuru wanadamu au mifugo wanapovikanyaga vijisilaha ovu hivi. Hali hii inahatarisha maisha ya raia wasiokuwa na taarifa ya kwamba sehemu ya eneo lao la nchi, limeambukizwa na vijibomu vya klasta.

Miongoni mwa wawakilishi waliohudhuria mkutano wa Oslo kutia sahihi Mkataba wa Kupiga Marufuku Mabomu ya Mtawanyo ya Klasta, kutokea Afrika Mashariki, alikuwemo Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kenya, Richard Onyonka. Redio ya UM ilifanya mahojiano na Waziri Onyonka.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao