Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa KM kwa Maziwa Makuu aripoti mafanikio haba kwenye mazungumzo ya upatanishi kwa JKK

Mjumbe wa KM kwa Maziwa Makuu aripoti mafanikio haba kwenye mazungumzo ya upatanishi kwa JKK

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Masuala ya Maziwa Makuu, Raisi mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo kwenye taarifa aliotoa Ijumatano kuhusu mazungumzo ya upatanishi – kati ya Serikali ya JKK na kundi la waasi la CNDP – yaliofanyika wiki hii mjini Nairobi, alisema juhudi zao, yeye binafsi akijumuika na Mpatanishi wa UA, Raisi mstaafu Benjamin Mkapa wa Tanzania, za kuendeleza makubaliano juu ya mfumo na kanuni za mazungumzo hakika, juhudi hizo ziliwapatia mafanikio haba sana.