Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unaadhimisha miaka 60 ya utetezi wa Haki za Binadamu

UM unaadhimisha miaka 60 ya utetezi wa Haki za Binadamu

Wiki hii UM uliadhimisha miaka 60 ya kupitishwa kwa Azimio la Mwito wa Kimataifa juu ya Haki za Binadamu, ambayo husherehekewa kila mwaka mnamo tarehe 10 Disemba. ~

Azimio hilo liliptishwa na Baraza Kuu la UM katika katika 10 Disemba 1948. Tangu wakati huo hadi hivi sasa, umma wa kimataifa ulibahatika kushuhudia maendeleo kadha wa kadha, kwenye juhudi za kutetea na kutekelezea raia wa ulimwenngu haki za binadamu, katika sehemu mbalimbali za dunia. Lakini juu ya maendeleo hayo, UM unasema bado kuna dosari kwenye utekelezaji hakika wa haki za binadamu, na kazi kubwa babdo imesalia kufanyika, kukamilisha utekelezaji wa haki za kibinadamu kama ilivyokusudiwa na waratibu wa Azimio.

KM Ban Ki-moon na maofisa wengine wa kimataifa wanafafanua maoni yao kuhusu suala hili kwenye makala hii ya wiki.

Sikiliza taarifa kamili kwenye idhaa ya mtandao.