"2009 unaashiria mizozo ziada", kuonya KM kwenye mkutano na wanahabari kufunga mwaka

17 Disemba 2008

Leo asubuhi, KM Ban Ki-moon alifanyisha kikao maalumu cha kufunga mwaka, na waandishi habari wa kimataifa katika Makao Makuu ya UM. Aliashiria kazi za UM katika mwaka 2009 zitafuatana na ugumu utakaovuka matatizo ya mwaka huu:~

KM alielezea mizozo kadhaa iliouvaa ulimwengu mwaka huu, ikijumlisha vurugu linaloendelea katika jimbo la Sudan magharibi la Darfur, mgogoro ulioselelea Mashariki ya Kati, hali ya Iraq, machafuko katika Usomali, mtafaruku wa Zimbabwe na mazingira ya Afghanistan, pamoja na kusailia matatizo mengine yanayohusu athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni. KM alisema alifurahika na kuridhika na ushirikiano uliokuwepo miongoni mwa Mataifa Wanachama katika kukabiliana na mzozo ulioletwa na mzoroto wa shughuli za uchumi duniani.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter