Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IMO yanasihi uvumilivu kwa wahamaji wa kimataifa

IMO yanasihi uvumilivu kwa wahamaji wa kimataifa

Tarehe ya leo, 18 Disemba 2008, inaadhimishwa kuwa ni Siku ya Kimataifa kwa Wahamaji.

Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) ameuzindua umma wa kimataifa ya kuwa “wahamaji wote, bila kujali hamasa inayowatoa makwao, au hadhi ya kisheria walionayo, wanawajibika kupatiwa hifadhi na ulinzi wa haki zao za kimsingi, kwa kulingana na mikataba ya kimataifa juu ya haki za binadamu.”