Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

WHO imeripoti hivi sasa wataalamu wa idara zinazohusika na matibabu ya magonjwa ya miripuko, wamejumuika na Wizara ya Afya na washiriki wengine wa kimataifa, kuratibu miradi maalumu itakayoongozwa na Kituo cha Udhibiti wa Kipindupindu, kwa madhumuni ya kuhudumia bora sekta ya afya ili kukomesha, halan, uenezaji wa maradhi nchini. Kwa mujibu wa taarifa ya WHO sekta ya

Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) Ijumaa limesaidia kupeleka kombania moja ya wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (FARDC) katika eneo la kaskazini-mashariki, baada ya kupokea taarifa, zenye uhakika, ya kuwa wafuasi fulani wa kundi la waasi wa Uganda wa LRA waliuwa kihorera wanakijiji 15, baada ya kukimbia shambulio la pamoja la vikosi vya JKK, Uganda na Sudan Kusini. Kwa mujibu wa ripoti za UM vikosi vya aina tatu vya wanajeshi wa JKK/Uganda/Sudan viliendeleza operesheni za kuwatoa mafichoni waasi wa LRA waliokuwa wamesakama katika bustani ya mbuga ya taifa, iliopo kaskazini-mashariki, waasi ambao baada ya kufuatilia mashambulio hayo walielekea Faradje, kilomita 120 mashariki ya Dungu na kuendeleza vitendo vya kikatili kwa kuua kihorera wanakijiji 15, kuharibu makazi na kujisaidia mali za wizi. Afisa Mnadhimu Mkuu wa vikosi vya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) aliiomba UM msaada wa usafiri wa kupepeleka vikosi vya taifa vya FARDC kwenye eneo husika ili kuzuia mashambulio mengine ya waasi. MONUC imeripoti kwamba Ijumamosi itapeleka kombania ya pili ya vikosi vya FARDC kwenye mji mwengine wa Haut-Uélé , ambapo kundi jengine la waasi wa LRA wamegundulikana kuendeleza mashambulio haramu dhidi ya raia.

Ofisi ya Mratibu Maalumu wa UM juu ya Mpango wa Amani kwa Mashariki ya Kati (UNSCO) imeripoti malori 105 yaliochukua shehena ya chakula na vifaa vya afya na matibabu, ikijumlisha malori 40 ya mashirika ya UM yenye kuhudumia misaada ya kiutu, yaliruhusiwa Ijumaa, (26 Disemba 2008) kuingia kwenye eneo liliokaliwa kimabavu la WaFalastina katika Tarafa ya Ghaza. Miongoni mwa vitu vilivyoruhusiwa kuingia Ghaza leo ilikuwa ni pamoja na : malori sita yaliochukua unga na chumvi, bidhaa za Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP); malori matatu yaliobeba vifaa vya afya vya Shirika la Afya Duniani (WHO); na malori matatu ya Shirika la UM lenye kufarajia kihali wahamiaji wa KiFalastina (UNRWA) yaliokuwa yamebeba shehena ya mchele na maziwa. Kuhusu nishati, Ofisi ya UNSCO imeripoti kuliruhusiwa na vikosi vya Israel kuingia Ghaza lita 428,000 za gesi ya viwandani na karibu tani 75 za gesi ya kupikia – lakini petroli na dizeli hazikuruhusiwa kuingia Ghaza. Kwa sababu hiyo kinu cha taa cha Ghaza kilimudu kuendesha jenereta moja tu, tabo ambayo itahitajia nishati ziada kabla ya Ijumapili kufanya kazi.

KM Ban Ki-moon ametangaza, kwa kupitia msemaji wake, kwamba ni matumaini yake kutabuniwa Kamisheni Huru ya Uchunguzi juu ya mauaji ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Pakistan, Beanazir Bhutto yaliotokea mwaka uliopita. Taarifa hiyo ilidhihirishwa leo Ijumaa, mwaka mmoja tangu marehemu Bhutto kuuawa. Risala ilisema KM ameshashauriana na Srikali ya Pakistna kuhusu mfumo na madaraka ya Kamisheni hiyo katika uchunguzi wa kuwatambua nani hasa waliohusikana na mauaji hayo na kuwafikisha mahakamani.