Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Karen Abu Zayd, Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linalofarajia Misaada ya kwa Wahamiaji wa KiFalastina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA), pamoja na Robert Serry, Mratibu Maalumu wa UM juu ya Mpango wa Amani Mashariki ya Kati (UNSCO) wamemtumia Waziri wa Ulinzi wa Israel, Ehud Barak, barua ya dharura, ya pamoja, yenye malalamiko makali dhidi ya matukio mawili ya “kushtusha” katika Tarafa ya Ghaza kuhusu usalama wa wafanyakazi wa UM na majengo yao, na barua iliomba Serikali ya Israel iipatie UM maelezo ya waziwazi juu ya matukio hayo.~

Tukio la pili lilijiri Ijumatatu ya leo ambapo Makao Makuu ya Ghaza ya Ofisi ya UM juu ya Mpango wa Amani kwa Mashariki ya Kati (UNSCO) yaliharibiwa na kubomolewa, pale makombora mawili ya vikosi vya Israel yalipopigwa karibu na nyumba ya wageni ya Raisi. Uchunguzi wa awali wa watumishi wa UM waliopo kwenye eneo hilo unasema sehemu iliopigwa makombora ilikadiriwa kuwa baina ya mita 20-30 kutoka majengo ya UNSCO. Chumba cha mkutano cha UNSCO katika Ghaza kiliharibiwa vibaya kabisa, pamoja na ofisi kadhaa za wafanyakazi; magari saba yaliangamizwa, kwa sehemu au kabisa; wakati mapaa, madirisha, milango, mabomba ya maji, waya za umeme na waya za mtandao wa mawasiliano ya kompyuta zote ziliharibiwa. Kwa bahati, ofisa mmoja mtaalamu, mzalendo, pamoja na walinzi watatu wa usalama waliwahi kukimbia na kujinusuru dhidi ya athari za makombora.

Umoja wa Mataifa unachukua hatua zote kuhakikisha watumishi wake, po pote walipo, huwa wanapata ulinzi unaofaa. UM katika Ghaza kwa sasa hivi unaendeleza shughuli zake ingali ina idadi ndogo sana ya wafanyakazi.

Kwa mujibu wa barua iliotumiwa Wizara ya Ulinzi Israel, serikali ilikumbushwa ya kuwa kisheria majengo ya UM ni lazima yalindwe na kuhifadhiwa. Barua ilisisitiza ya kwamba Serikali ya Isarel inazo taarifa kamili kuhusu plani hakika ya majengo ya UM katika Ghaza. Mashambulio ya makombora ya vikosi vya Israel kwenye majengo hayo yamefurutu ada za kimataifa, na maadili ya UM, na yametukia bila ya onyo. Mashambulizi haya ya kijeshi kwenye hali ya uhasama na vurugu, karibu na maeneo ya UM, hujumu ambazo zinahatarisha watumishi wa UM, pamoja na majengo yake, ni lazima yakomeshwe, halan, na yasirduidiwe tena, barua ilisisitiza. Bi Abu Zayd pamoja na Bw Serry wameitaka Serikali ya Israel wakamilishe haraka kadhia hii.

Ofisa wa kijeshi anayofanya kazi na Shirika la Vikosi Mseto vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) amefariki Ijumatatu, baada ya kupigwa risasi mguuni Ijumamosi usiku, pale gari yake ilipotekwa nyara kwenye soko la ElFasher katika Darfur Kaskazini. Maerehemu huyu alikuwa miongoni mwa maofisa watatu wa vikosi vya UNAMID walioibiwa gari na majambazi watatu wasiojulikana. Maofisa wa UNAMID walilazimishwa kutoka kwenye gari lao, na wakati wakijaribu kufanya hivyo mmoja wa maofisa alipigwa risasi. Baada ya tukio hilo majambazi walikimbia shoti na gari wakielekea sehemu ya kaskazini.