Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

KM ametoa taarifa maalumu, kwa kupitia msemaji wake, iliolaani vikali vitendo vya ukatili wa kukirihisha, ulioripotiwa kufanywa majuzi na waasi wa kundi la LRA katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) na sehemu za Sudan Kusini. KM amesisitiza wafuasi wa LRA wanalazimika kuhishimu na kufuata

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imewasilisha ripoti mpya kuhusu tatizo la miripuko ya kipindupindu katika Zimbabwe, taarifa yenye kuonyesha jumla ya vifo viliyotokana na ugonjwa huo sasa hivi ni sawa na watu 1,608, na watu 30,000 ziada waliripotiwa kuambukizwa nchini. Mnamo siku za karibuni, Shirika la Afya Duniani (WHO) limetayarisha timu ya wataalamu wa kuhudumia, kidharura, miripuko ya kipindupindu Zimbabwe, ikijumuisha ofisa wa afya ya mazingira, wataalamu wanaoshughulikia magonjwa ya miripuko na wasimamizi wa fani ya takwimu. Kadhalika, WHO imo mbioni kuanzisha Kituo cha Uongozi na Udhibiti wa Kipindupindu katika eneo husika. Shirika la UNICEF, kwa upande wake, limepeleka Zimbabwe sasa hivi, kutokea Afrika Kusini, kwa kutumia ndege na malori, misaada ziada inayojumuisha madawa ya matibabu, aina ya chumvi za kukomesha mtu kuharisha, mirija ya ukunga pamoja na vifaa vya tiba ya uzazi.

Kwa mara ya kwanza, tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa UM juu ya Maafa ya Dharura au Mfuko wa CERF, Mataifa Wanachama yalifanikiwa mawaka huu kutimiza lengo lao la kukusanya, kwa wastani, dola milioni 450 kwa mwaka. Katika 2008, Mataifa Wanachama 81 pamoja na wahisani kadha wa kimataifa walichangisha jumla ya dola milioni 452.5 kufadhilia Mfuko wa CERF. Mataifa wahisani yalioongoza katika kuchangisha msaada huo yalikuwa Uingereza($80 milioni), Uswidin ($56 milioni), Norway ($55 milioni) na Uspeni ($44 milioni). Wachangishaji wakubwa wa binafsi waliwakilisha kampuni ya huduma za wataalamu ya PricewaterhouseCoopers, ambayo ilifadhilia dola 500,000. Mfuko wa CERF ulianzishwa mwaka 2006 na Baraza Kuu la UM kwa dhamira ya kuwasaidia watu walioathirika na maafa ya ghafla, pamoja na wale wanaojikuta kwenye dharura zilizozorota, kwa kuwapatia huduma za haraka, zinazoaminika na bila ya upendeleo zitakazosaidia kuwavua na majanga hayo. Tangu Mfuko wa CERF kubuniwa, miradi ya dharura katika nchi 67 ilihudumiwa dola bilioni 1.1 kukidhi mahitaji ya umma waathirika wa maafa.