Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Ofisi ya Msemaji wa KM imeripoti kwamba Ban Ki-moon anaendelea kushauriana, kwa kutumia njia ya simu, na maofisa wa UM wa vyeo vya juu waliokuwepo kwenye eneo la uhasama Mashariki ya Kati. Katika saa 24 zilizopita KM aliwasiliana na mawaziri wa nchi za kigeni wa Israel na Marekani, na KM anatazamiwa kuongeza juhudi zake katika siku zijazo katika kuhakikisha mwito wa kusimamisha mapigano katika eneo liliokaliwa la WaFalastina katika Tarafa ya Ghaza utahishimiwa.

Shirika la UM Linalofarajia Wahamiaji wa KiFalastina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) limeanzisha kampeni ya kuchangisha msaada wa dharura wa dola milioni 34 kukidhi mahitaji ya umma ulioathirika na mashambulio yanayoendelezwa na vikosi vya Israel katika Ghaza. Ombi hili linajumlisha mchango ziada tofauti, na lile ombi la mwanzo wa mwezi Disemba la kutaka UNRWA ifadhiliwe Msaada wa Dharura kwa 2009 wa dola milioni 275 kuhudumia wakazi wa maeneo yaliokaliwa ya WaFalastina.

Wakati huo huo, Radhika Coomaraswamy, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Watoto kwenye Mazingira ya Uhasama, alisema kwenye taarifa aliodhihirisha Ijumatano ya kuwa hali hivi sasa katika Ghaza ni isiovumilika wala kustahamalika, kwa wakazi raia, hususan miongoni mwa watoto wadogo. Coomaraswamy amerudia tena mwito wake uyatakayo makundi yote ya WaFalastina kuchukua kila hatua inayohitajika kuwakinga watoto dhidi ya athari za vurugu, na kuhadharisha watoto wasishirikishwe, aslant, kwenye mapigano.

UM umethibitisha wanajeshi 12,374 wa kutumikia vikosi mseto vya UM/UA kwa Darfur, yaani vikosi vya UNAMID, wameshawasili Sudan kwa sasa. Idadi hiyo inajumlisha asilimia 63 ya wanajeshi 19,555 waliodhaminiwa na Baraza la Usalama kuenezwa kwenye jimbo la uhasama katika Sudan magharibi. Tarehe ya leo, 31 Disemba 2008, UNAMID inaadhimisha mwaka mmoja tangu kuanza operesheni zake katika Darfur. KM amepongeza zile nchi zilizochangia wanajeshi wake kwa UNAMID, na pia kuupongeza mchango wa Serikali ya Sudan, wa miezi ya karibuni, uliorahisisha wanajeshi hawo kuenezwa Darfur kama ilivyodhaminiwa na jumuiya ya kimataifa.

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetoa onyo ya kuwa kuongezeka kwa mapigano na mikwaruzano katika eneo la mashariki la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) ni vitendo vinavyopalilia uharamishaji mkubwa wa haki za watoto na wanawake. UNICEF iliihadharisha jumuiya ya kimataifa kutopuuza hyali hii mbaya iliokabili wanawake na watoto katika JKK. UNICEF imeripoti vitendo vya ukandamizaji na matumizi ya nguvu yanaendeleezwa na kusambazawa katika vijiji, ambapo wakiukaji wa haki hizo kutokhofu adhabu, hasa dhidi ya wahamiaji wa ndani waliopo katika yale maeneo ya mastakimu ya muda. UNICEF imesema ipo tayari kuwapatia hifadhi wale watoto waliolazimishwa kushiriki kwenye mapigano, ambao walikimibia makundi ya waasi. UNICEF imesema hivi sasa inawasaidia watoto 31, waliowatoroka waasi wa LRA, kupata hifadhi kinga.