Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walimwengu wanasailia matumizi salama mbadala dhidi ya DDT kupiga vita Malaria

Walimwengu wanasailia matumizi salama mbadala dhidi ya DDT kupiga vita Malaria

Wajumbe 80 wanaowakilisha serikali, viwanda na makarkhana, pamoja na taasisi za kufanyia utafiti na vile vile mashirika yasio ya kiserikali wamejumuika hii leo Geneva kuhudhuria kikao cha siku tatu kujadilia gharama za kutumia dawa mbadala na DDT, kemikali ambayo hutumiwa kuua vijidudu vya malaria, na yenye kuathiri vibaya afya ya wanadamu.