Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yahadharisha: "Unyamavu wa kigeugeu umewasili Goma"

UNICEF yahadharisha: "Unyamavu wa kigeugeu umewasili Goma"

Hali inaendelea kuwa shwari katika Goma, lile eneo la mashariki katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, ambapo mnamo siku za karibuni mapigano makali yalishtadi huko baina ya vikosi vya serikali na waasi wa kundi la CNDP.

Hali katika Goma kwa hivi sasa ni tulivu. Inaelekea hali ya maisha inaanza kurejea kuwa ya kawaida.” Aliendelea kusema licha ya kuwa hali ni shwari bado wasiwasi umetanda Goma … na inaonekana watu wengi wamechanganyikiwa woga. Kwa mujibu wa Msemaji wa UNICEF hali hii ya kigeugeu inaweza kubadilika na kuharibika mara moja, kama ilivyotukia katika siku za nyuma; baadhi ya wakati hali huonekana kuwa tulivu, halafu ghafla linazuka vurugu. Kwa hivyo, alihadharisha, hali hairidhishi na bado haijatulia kihakika. Murthy vile vile alisema msafara wa malori 12 ya UM, yaliyoongozwa na vikosi vya Shirika la Ulinzi Amani katika JKK (MONUC), yaliochukua shehena za madawa na tembe za kusafishia maji ya kunywa, umefanikiwa kuwasili Rutshuru, Kivu Kaskazini, eneo linalodhibitiwa hivi sasa na wafuasi waasi wa Laurent Nkunda. Madawa haya yanatarajiwa kuhudumia matibabu wahamiaji wa ndani 250,000 waliong’olewa makazi kwa sababu ya mapigano. Taarifa za MONUC zinasema Mawaziri wa Nchi za Nje wa Ufaransa na Uingereza, yaani Bernard Kouchner na David Miliband, wanaozuru eneo la Maziwa Makuu kwa sasa, wanajaribu kushirikiana na mataifa jirani na JKK kurudisha utulivu na amani kwenye eneo la vurugu, haraka iwezekanavyo.