Skip to main content

KM asailia uchaguzi Marekani

KM asailia uchaguzi Marekani

Hii leo, tarehe 04 Novemba (‘08) makumi milioni ya raia wa Marekani wanashiriki kwenye kura ya kuteua raisi mpya.

"Kuhusu mimi, kama KM, nipo tayari, na nimeshajiandaa kufanya kazi, kwa ukaribu zaidi na Raisi mpya wa Marekani,yeyote atakayechaguliwa.” Alisema tangu alipochukua wadhifa wa KM, moja ya mambo aliyoyapa umuhimu zaidi ni ile rai ya kudumisha na kuimarisha ushirikiano mwema, na wenye nguvu, na wa karibu zaidi baina ya Marekani na UM, kwa sababu aliamini, yeye binfasi, na kwa kulingana na taratibu rasmi za kikazi, kwamba ni muhimu, na tunawajibika, kuendeleza uhusiano mzuri na serikali ya taifa mwenyeji, taifa ambalo ndilo lenye kutoa mchango mkubwa katika UM, na hasa ilivyokuwa Marekani ni moja ya mataifa makuu yenye kuongoza duniani. Alisisitiza KM ya kwamba, kwa kuambatana na hoja hizo, ana hakika ataweza kuimarisha ushirikiano mzuri zaidi baina ya serikali mpya ijayo ya Marekani na UM.