Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

KM ameshtumu, kwa uzito mkubwa, utoroshaji uliotukia leo Ijumatano kwenye uwanja wa ndege karibu na mji wa Dusamareb, Usomali wa wahudumia wanne wa misaada ya kiutu pamoja na marubani wawili. KM alitaka wafanyakazi hawo waachiwe haraka, na alibainisha kuwa na wasiwasi juu ya mtindo ulioshtadi katika eneo hilo la kuteka nyara wahudumia misaada ya kihali na halafu kuwaua. Alitoa mwito unayoyataka makundi yote kutambua watumishi wa kimataifa katika kazi zao hawapendelei upande wowote, na alihimiza waruhusiwe kuendeleza shughuli za kunusuru maisha ya mamilioni ya Wasomali, ambao jumla yao inakaribia nusu ya idadi ya watu nchini.~

Edmond Mulet, Naibu KM juu ya Operesheni za Amani za UM aliwakilisha katika Baraza la Usalama ripoti ya KM juu ya utekelezaji wa Mapatano ya Amani kwa Sudan. Alisema maafikiano ya kusitisha mapigano yanahishimiwa, hali ya sualama, kwa ujumla, ni shwari Sudan kusini na kwenye vituo vya mpito, ikijumlisha Abyei. Alisema kuna haja ya dharura kulenga juhudi za jamii ya kimataifa kuyawezesha makundi husika kufanya kura ya moani na kuhakikisha utulivukatika 2011 na baadaye.

Ujumbe wa UM unaosimamia Mfuko wa Ujenzi wa Amani umeanza ziara ya wiki moja katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), iliyoongozwa na Mwakilishi wa Kudumu wa Ubelgiji. Tume itafanya mikutano ya ushauri na wadau muhimu kadha pamoja na maofisa wa Serikali ili kusailia nao mahitaji ya kuimarisha amani katika nchi na mchango wa wahisani wa kimataifa unaotakiwa kuyatekeleza hayo.