Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUC imeripoti mapigano kufumka tena karibu na Rutshuru

MONUC imeripoti mapigano kufumka tena karibu na Rutshuru

Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limetangaza taarifa yenye kulaani vikali kufufuliwa tena kwa mapigano katika eneo karibu na mji wa Rutshuru, kwa siku ya pili mfululizo, baina ya waasi wa CNDP walio wafuasi wa Laurent Nkunda, na vikosi vya wanamgambo wa kundi la PARECO na lile la Mayi Mayi.