Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wapatanishi wa Mashariki ya Kati wana matumaini kuhusu amani

Wapatanishi wa Mashariki ya Kati wana matumaini kuhusu amani

KM Ban Ki-moon alitoa taarifa maalumu, kwa niaba ya wawakilishi waliohudhuria mkutano wa wapatanishi wa pande nne juu ya mzozo wa Mashariki ya Kati, uliofanyika Sharm El Sheikh, Misri mwisho wa wiki, taarifa iliobainisha ya kuwa Wafalastina na Waisraili wameafikiana kwamba hawatofanikiwa kuwasilisha makubalianao ya amani mpaka masuala yote husika yatakaposuluhishwa kati yao.