Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwenye kikao cha kila mwezi na waandishi habari KM azingatia mizozo ya kimataifa, ikijumlisha vurugu la JKK

Kwenye kikao cha kila mwezi na waandishi habari KM azingatia mizozo ya kimataifa, ikijumlisha vurugu la JKK

Leo Ijumanne, KM Ban Ki-moon leo alikuwa na mahiojiano ya kila mwezi na waandishi habari wa kiamataifa waliopo hapa Makao Makuu. Kwenye mkusanyiko huo KM alisailia juhudi za karibuni za kukabiliana na mgogoro wa fedha katika soko la kimataifa, pamoja na kuzingatia matatizo ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Kuhusu hali katika JKK KM alisema UM umejikuta kunaswa kwenye mazingira ya kigeugeu na jazba itakayochochea hali ya hatari kuvamia, sio JKK pekee bali eneo zima la Maziwa Makuu. Alisema licha ya kuwa mkutano wa kikanda ulioandaliwa na Umoja wa Afrika mjini Nairobi mwisho wa wiki iliopita ulitoa mwito muhimu unayoyataka makundi yote yenye silaha Kivu Kaskazini kusimamisha mapigano, halan, hata hivyo UM bado unapokea ripoti zinazoelezea kuendelea kwa mapigano ya hapa na pale miongoni mwa makundi yanayohasimiana na dhidi ya raia, halkadhalika. Kwa kutokana na hali hiyo, KM alihadharisha wahusika wa mapigano hayo kama ifuatavyo:

“Ninakhofia ripoti tulizopokea zinaonyesha dhahiri wapiganaji wameshiriki kwenye mauaji ya kihorera dhidi ya raia, umma ambao vile vile umetendewa karaha ya kunajisiwa na wakati huo huo kunyanganywa mali zao.” KM aliyaakumbusha makundi yote husika na mapigano katika mashariki ya JKK ya kwamba kila wanapokiuka kanuni za vita na mapigano, huwa wanajitwika dhamana ya kibinafsi na huchukua, kisheria, dhamana ya makosa hayo ya jinai ya vita, hususan kwa wale wenye vyeo na madaraka ya kuongoza na kutawala wafuasi wao kwenye mazingira kama hayo ya vurugu.