UNICEF imearifu kuwasili misaada ya madawa Goma
Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limearifu kuwasili Goma, mnamo Ijumatatu na Ijumanne, kwa ndege nne zilizochukua shehena ya madawa kinga dhidi ya maradhi kipindupindu na dhidi ya maambukizo yanayoathiri uvutaji pumzi.