Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahudumia misaada ya kiutu Lubero Kusini wasitisha shughuli kutokana na ukosefu wa usalama

Wahudumia misaada ya kiutu Lubero Kusini wasitisha shughuli kutokana na ukosefu wa usalama

Ofisi ya UM inayohusika na Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti mashirika yenye kuhudumia misaada ya kiutu katika eneo la mapambano la JKK, hasa katika Lubero Kusini, yamelazimika kuhamisha wafanyakazi wao kwa sababu ya kutanda kwa hali ya wasiwasi kieneo.

“Kuna eneo, katika Lubero kusini, ambalo tunaweza kusema kwa sasa huko, hali kidogo ni tulivu na eneo ambalo tunaweza kulifikia. Lakini hata hivyo, tumelazimika tusitishe huduma zetu, kwa muda, katika eneo hilo kwa sababu ya hali ya wasiwasi iliopamba. Mashirika kadha yanayohusika na huduma za kiutu yamebidi yachukue hatua kinga, na yameamua kuondoka kabisa kwa sababu ya hali ya wasiwasi na kigeugeu iliojiri hapo, hali ambayo hairuhusu mashirika yanayogawa misaada ya kiutu kuendeleza shughuli zao kwa utulivu wa amani. Mzoroto huu wa huduma za kiutu kama haujadhibitiwa mapema, utaendelea kupanuka na kuhatarisha maisha ya umma waathiriwa waliong’olewa makazi, ambao idadi yao kwa sasa inakadiriwa baina ya watu 252/253.”