Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa yameahidi kushirikiana kupiga vita kuvu wanaoharibu ngano

Mataifa yameahidi kushirikiana kupiga vita kuvu wanaoharibu ngano

Mkutano ulioandaliwa bia na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) pamoja na Serikali ya Bara Hindi na washiriki wengine wa kimataifa, kuzingatia namna ya kudhibiti bora ugonjwa wa kuvu wanaoharibu mashina ya mimea ya ngano, ulimalizika kwa kutoa mwito maalumu uliohimiza Mataifa Wanachama kuchukua hatua za haraka kulikomesha tatizo hili kipamoja.