Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu linasailia utamaduni wa amani

Baraza Kuu linasailia utamaduni wa amani

Baraza Kuu la UM leo limeanzisha majadiliano ya jumla, ya siku mbili, kwenye kikao cha wawakilishi wote, kuzingatia namna dini mbalimbali zitatumia kile kilichotafsiriwa kama “Utamaduni wa Amani” kusaidia umma wa kimataifa kutatua, kipamoja, yale masuala yanayodhalilisha ubinadamu, mathalan, umaskini na njaa.

“Kwa amani kudumu, wanadamu, makundi ya kimataifa na pia Mataifa ni lazima kuhishimiana na kuelewana.” Alisema majadiliano ya katika Baraza Kuu, miongoni mwa wafuasi wa dini mbalimbali yanazingatia kihakika haja hii kuu, kwa nguvu zaidi na kwa marudio. KM alikumbusha mkutano huu wa kihistoria umefanikiwa kujumuisha kwenye Makao Makuu wafuasi kadha wa dini kuu za dunia, pamoja na wanazuoni mashuhuri, wasomi na wadau wengine ambao kuwepo kwao kumethibitisha maadili ya kimsingi, kuhusu usawa wa wanadamu wote, “bila kujali rangi, ukabila, ubaguzi, dini wala urithi wa utamaduni.”