Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mihogo isioambukizwa virusi haribifu yafaidisha lishe kwa wakazi wa Maziwa Makuu: FAO

Mihogo isioambukizwa virusi haribifu yafaidisha lishe kwa wakazi wa Maziwa Makuu: FAO

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limeripoti kupatikana mafanikio makubwa karibuni katika kupambana na vijidudu vinavyoharibu mazao ya mihogo katika mataifa ya Afrika yaliozunguka eneo la Maziwa Makuu, ikijumlisha Burundi, JKK, Rwanda na Uganda.