Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 50,000 ziada karibu na Goma wahudumiwa chakula na WFP

Watu 50,000 ziada karibu na Goma wahudumiwa chakula na WFP

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) Ijumanne limeanza kugawa posho ya chakula cha siku 20 kuhudumia watu 56,000 waliopo kwenye kambi tatu za wahamiaji waliong’olewa makazi, kwenye vitongoji vya mji wa Goma.

“Leo tumeanzisha ugawaji wa posho ya chakula cha siku 20,kwa watu zaidi ya 56,000 waliopo kwenye kambi tatu karibu na Mji wa Goma: yaani zile kambi za Mugunga ya Kwanza na Mugunga ya Pili, na kambi ya Bulenga, huduma ambazo zitafuatiliwa baadaye na ugawaji kwenye tatu nyengine katika Goma. Vile vile hii leo tunagawa misaada ya chakula kwa watu waliong’olewa makazi 25,000 waliopo katika eneo la Kitchanga, na pia kuwapatia posho ya chakula, mnamo siku nne zijazo, watu 11,000 waliopo sehemu ya Kilolirwe; maeneo yote haya mawili sasa hivi yapo chini ya kundi la waasi la Laurent Nkunda. Kadhalika WFP iatagawa chakula kwa watu 93,000, waliohamishwa kidharura makazi, na pia kufadhilia wenyeji wao msaada huo, katika Rutchuru kwenye eneo la Kiwanja, na ugawaji huo utaendelea mpaka mwisho wa Ijumatano. Zaidi ya hilo, kwa ushirikiano na Kamati ya Kimataifa ya Msaaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (ICRC), tunajiandaa leo hii kuwapatia chakula watu 50,000 waliohamishwa makazi katika maeneo ya Sake na Miniova … Huduma hizi zitaendeshwa kwa mategemeo hali ya usalama itaendelea kuwa shwari na ugawaji wa chakula utaendelea kupatiwa ulinzi wa vikosi vya amani vya MONUC.”