19 Novemba 2008
Hii leo kwenye mji mkuu wa Moroni, wa Masiwa ya Comoros kumeanza mkutano wa siku tatu, unaohudhuriwa na wataalamu wa kimataifa wanaohusika na fani ya volkeno, na wale wanaohusika na utumiaji wa busara wa mali ya asili na udhibiti wa maafa ya kimaumbile.