Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelezo mafupi juu ya hali katika JKK

Maelezo mafupi juu ya hali katika JKK

Hii leo asubuhi Baraza la Usalama limekutana kuzingatia azimio liliowakilishwa na Ufaransa kuhusu uwezekano wa kuongeza wanajeshi 3,000 ziada wa kimataifa, wanaohitajika kuimarisha ulinzi wa amani katika JKK, kufuatia mapigano yaliopamba kwenye eneo hili la Maziwa Makuu mnamo wiki za karibuni.~

KM ameyahimiza makundi yote yaliohusika na mgogoro wa Kongo mashariki kuhishimu mapatano yao ya kusimamisha uhasama, na kuwaomba wahakikishe kunakuwepo usalama wa misaada ya kiutu inayopelekwa kwenye eneo la mgogoro, na pia kuwahimiza waendelee kushiriki kwenye juhudi za kutafuta suluhu ya kuridhisha ya kisiasa juu ya mfarakano wao.

Kwenye mkutano wa kila wiki na waandishi habari Shirika la Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limeripoti baadhi ya makundi ya waasi wa CNDP, Ijumatanao usiku walianza kueneza tena askari wao kwenye zile sehemu za Kanyabayonga-Nyanzale na Kabasha-Rutshuru, kufuatia tangazo la upande mmoja, liliotolewa kabla, liliodaia linarudisha nyuma wapiganaji wao. MONUC imeanzisha doria kadha kuthibitisha hali halisi ilivyo kwenye ardhi ya maeneo husika.