Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kipindupindu kimekithiri Zimbabwe,OCHA yaonya

Kipindupindu kimekithiri Zimbabwe,OCHA yaonya

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeonya ya kwamba maradhi ya kipindupindu yameonekana kukithiri, kwa kasi, mnamo siku za karibuni nchini Zimbabwe.

“Idadi ya watu walioambukizwa na kipindupindu nchini Zimbabwe, katika siku za karibuni, imeongezeka kutoka wagonjwa 6,072 hadi 7,283 – huu ni muongezeko wa wagonjwa 1,211. Wakati huo huo, vifo vya wagonjwa wa kipindupindu Zimbabwe navyo pia vimekithiri, kutoka jumla ya watu 294 na kufikia 313 – takwimu ambazo zilikusanywa kumalizikia tarehe 20 Novemba. Maeneo ambayo yamesibika zaidi na maradhi haya yanajumlisha pia yale ya Mutare na Chimanimani katika Manicaland, na vile vile zile sehemu za Guruve na Concession ziliopo Mashonaland ya Kati; vile vile waathiriwa wa kipindupinndu wamekutikana katika maeneo ya Masvingo na Midlands. Eneo lilioshuhudiwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa maradhi hayo ni lile la Budiriro, karibu na mji mkuu wa Harare, na vile vile maradhi yamekutikana kwenye ile sehemu ilipo daraja maarufu ya Bay Bridge, inayounganisha Zimbabwe na Afrika Kusini. Hali hii humaanisha wahudumia afya wa mataifa haya mawili wanashirikiana kw aukaribu zaidi kuhakikishia ugonjwa unadhibitiwa, ili usije ukaenea na kusambaa zaidi Afrika Kusini na kuhatarisha masiha ya umma kieneo.”