FAO imemtunukia Raisi wa Malawi 'Nishani ya Agricola' kwa kujitegemea chakula

28 Novemba 2008

Raisi wa Malawi, Bingu wa Mutharika ametunukiwa \'Nishani ya Agricola\' na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) kwa mchango wake muhimu katika kurekibisha uchumi wa kilimo nchini. Malawi siku za nyuma lilikuwa ni taifa lilioshuhudia uhaba mkubwa wa chakula. Lakini baada ya kujulishwa sera mpya ya kilimo Malawi imefanikiwa kuzalisha kiwango cha kujitosheleza cha chakula.

Raisi Bingu wa Mutharika Alkhamisi alikabidhiwa 'Nishani ya Agricola' na Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Jacques Diouf alipozuru mji mkuu wa Lilongwe, Malawi. Uchumi wa Malawi unaashiriwa kuongezeka kwa asilimia 8 katika 2008.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter