Skip to main content

Hali Usomali inatia wasiwasi: OCHA

Hali Usomali inatia wasiwasi: OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura na Huduma za Kiutu (OCHA) imeripoti mnamo wiki hii, raia karibu 80 waliuawa na zaidi ya watu 100 walijeruhiwa baada ya vikosi vya ulinzi amani vya Umoja wa Afrika (UNISOM) viliposhambuliwa kwenye mji wa Mogadishu na makundi yanayopinga serikali.

Kama mnavyoelewa mapigano yaliozuka karibuni Mogadishu yalisababisha ongezeko kubwa la kwa wahamiaji wa ndani, waliong’olewa makazi, ambao jumla yao inakadiriwa kuwa 15,000 – na wahamiaji hawa wa ndani, au IDPs, wanahitajia kupatiwa chakula, makazi ya muda na vile vile misaada ya jumla ya kimsingi. Idadi hii imeongezea ile ya wahamiaji wengine wa IDPs 300,000 wanaoishi kwenye eneo dogo la kilomita chache tu, hali ambayo inatota kwa sababu pia kuna upungufu wa fedha zinazotakiwa kukidhi mahitaji ya umma husika. Kati ya jumla inayotakiwa ya dola miloni 646 kuhudumia kihali Usomali, kuna upungufu wa posho muhimu ya dola milioni 231 ambazo zinatakikana kupatia asilimia 43 ya jumla ya idadi ya raia nchini Usomali – yaani sawa na watu milioni 3.2 (tatu na laki mbili) huduma za haraka za kiutu. Mchango huo ni wa mahitaji ya lazima na ni muhimu kufadhliwa OCHA haraka ili iweze kutekeleza huduma zake kama inavyopasa.”