Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM wakutana Zanzibar kuzingatia udhibiti bora wa maafa ya dharura Afrika

Wataalamu wa UM wakutana Zanzibar kuzingatia udhibiti bora wa maafa ya dharura Afrika

Wataalamu karibu 50 wanaohusika na utendaji wa miradi ya dharura, na ya kiutu, wa kutoka maeneo kadha ya Afrika, wakiwakilisha Shirika la Afya Duniani (WHO) walikutana kwa wiki moja, kuanzia Oktoba 06 kisiwani Zanzibar, Tanzania kufanya mapitio kuhusu namna mataifa ya Afrika yanavyotakiwa kujiandaa kukabiliana na maafa yanayoripuka mara kwa mara kwenye maeneo yao.