Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikosi vya polisi maalumu wa Indonesia vyawasili Darfur

Vikosi vya polisi maalumu wa Indonesia vyawasili Darfur

Kundi Maalumu la Polisi 130 kutoka Indonesia (FPU) limewasili jimbo la magharibi la Sudan mwisho wa wiki kwa ndege maalumu ya UM, kwa lengo la kuimarisha juhudi za ulinzi wa amani za vikosi vya mchanganyiko vya UM na UA kwa Darfur vya UNAMID. Madhumuni hakika ya vikosi vya UNAMID hasa ni kukomesha fujo kwenye eneo hilo la mzozo la Sudan.