Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM imeripoti waasi wa Uganda karibuni walipitisha mashambulio maovu katika JKK

UM imeripoti waasi wa Uganda karibuni walipitisha mashambulio maovu katika JKK

Ofisi ya UM juu ya Haki za Binadamu pamoja na Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika JKK (MONUC) wamewasilisha ripoti mpya ya pamoja iliothibitisha kihakika ya kwamba kuanzia kati ya mwezi Septemba mwaka huu, kundi la waasi wa Uganda wenye sifa mbaya linalojidai kuwa ni Jeshi la Upinzani la Mungu, au LRA, limeua zaidi ya watu 200 katika JKK.