Huduma za misaada ya kiutu Usomali zinaendelea kunywea, OCHA imeonya

14 Oktoba 2008

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kwamba mazingira ya kuhudumia misaada ya kiutu katika maeneo ya Kusini na Kati nchini Usomali yamenyweya zaidi wiki hii, kama anavyotueleza Elizabeth Byrs, msemaji wa OCHA, pale alipokutana na waandishi habari Geneva Ijumanne:~~

Hivi sasa, raia wa Usomali milioni 3.2 wanahitajia kufadhiliwa misaada ya dharura ya kihali, jumla inayowakilisha asilimia 43 ya iaddi ya watu nchini. Kadhalika, tusisahau pia tangu mwanzo wa 2008 wahudumia misaada ya kiutu 25 walitekwa nyara na majambazi na bado wameshikwa nao; na kipindi hicho hicho maharamia wameshashambulia mashua na boti zaidi ya 60 kwenye mwambao wa Usomali. Hali hii imesababisha shughuli kadha za mashirika yasio ya kiserikali kusitishwa, kwa muda, hasa lile shirika linalotoa misaada ya kiutu la kimataifa la CARE.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter