Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madai ya Georgia dhidi Urusi yapewa usikizi na Mahakama ya ICJ

Madai ya Georgia dhidi Urusi yapewa usikizi na Mahakama ya ICJ

Mahakama Kuu ya Kimataifa (ICJ) iliopo Hague, Uholanzi ilitazamiwa leo kutoa maamuzi yake juu ya madai ya Georgia ya kwamba Urusi ilikiuka kanuni za kimataifa kwa kuingiza vikosi vyake kwenye jimbo la Ossetia Kusini mnamo tarehe 07 Agosti mwaka huu.

Mahakama Kuu ya Dunia imepitisha maazimio ya muda kuambatana na kesi hiyo, ikiwemo lile pendekezo linaloyataka Mataifa ya Urusi na Georgia kujizuia na vitendo vyote vya ubaguzi wa rangi na pia kutakiwa waasifadhilia, wala kuhami, au kuunga mkono vitendo kama hivyo; na nchi hizi mbili zilitakiwa kurahisisiha huduma za misaada ya kiutu kwenye maeneo ya vurugu, na kuahidi kutobagua haki za Makundi yanayohusika na mvutano wao na wajizuie na vitendo vya kuzidisha au kurefusha uhasama baina yao.