Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la mzozo wa Georgia linachunguzwa na wawakilishi wa kimataifa Geneva

Suala la mzozo wa Georgia linachunguzwa na wawakilishi wa kimataifa Geneva

Mazungumzo ya kiwango cha kitaaluma kuhusu hali katika Georgia yameanza rasmi Geneva Ijumatano ya leo, yakihudhuriwa na wawakilishi wa UM, Umoja wa Ulaya, Jumuiya ya Ushirikiano na Usalama katika Ulaya (OSCE) na vile vile wajumbe wa kutoka Urusi, Georgia na Marekani.

Kikao cha mwanzo cha majadiliano juu ya Georgia kilihitimisha mazungumzo yake kwa wajumbe wa kimataifa kuafikiana kukutana tena tarehe 18 Novemba 2008.