Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la ulajirushwa Afrika lazingatiwa na mkutano uliodhaminiwa na UM

Tatizo la ulajirushwa Afrika lazingatiwa na mkutano uliodhaminiwa na UM

Kuanzia tarehe 13 Oktoba katika mji wa Addis Ababa, Ethiopia kulikusanyika wataalamu pamoja na wabuni sera za kitaifa na pia viongozi wa jamii za kiraia, kutoka nje na ndani ya Afrika, kwenye mkutano wa siku tatu uliodhaminiwa na UM kuzingatia taratibu za kuimarisha zaidi zile juhudi za kupiga vita janga la ulajirushwa barani Afrika.