Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bidii ya kisiasa inakosekana kufyeka njaa, FAO inahadharisha

Bidii ya kisiasa inakosekana kufyeka njaa, FAO inahadharisha

Kwenye taadhima za mjini Roma, Utaliana za Siku ya Chakula Duniani hii leo, kwenye tarehe ambayo Shirika la UM la Chakula na Kilimo (FAO) lilipoanzishwa katika 1945, Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Jacques Diouf aliwaambia wageni waliohudhuria taadhima hizo ya kwamba vifaa vipo na uwezo upo wa kufyeka milele tatizo liliokithiri la njaa ulimwenguni, hususan miongoni mwa ule umma unaosumbuliwa zaidi na njaa sugu ambao idadi yao imekadiriwa milioni 923.