Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP inahimiza tuwakumbuke, kihali na mali, waliochonotwa na kuumizwa na baa la njaa

WFP inahimiza tuwakumbuke, kihali na mali, waliochonotwa na kuumizwa na baa la njaa

Josette Sheeran, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) alikubaliana na fafanuzi za KM, na alikiri kwamba ni wajibu wa jumuiya ya kimataifa kuhakikisha msaada unapatikana kuhudumia kidharura tatizo linaloathiri kila siku aila kadha wa kadha ulimwenguni, yaani tatizo la chakula, licha ya kuwa mazingira ya mzozo wa fedha nayo pia yanaendelea kusumbua umma wa kimataifa.