'Mamilioni wanaotota njaa na ufukara wanahitajia misaada maridhawa kimataifa, halan' - KM Ban
Kwenye ujumbe aliotoa KM Ban Ki-moon yeye alilalama ya kwamba ‘Siku ya Chakula Duniani’ imewasili mwaka huu katika kipindi cha mgogoro mkubwa, ambapo machafuko yametanda kwenye soko la fedha la kimataifa, hali ambayo ilifanywa kuwa mbaya zaidi kwa sababu ya kupanda kwa bei za chakula na nishati duniani.