Hapa na Pale

21 Oktoba 2008

Ripoti ya KM kuhusu operesheni za vikosi vya mchanganyiko vya UM na UA kwa Darfur (UNAMID), iliotolewa leo hii, imebainisha kuwepo ukosefu wa mazingira yanayohitajika kuimarisha usalama na amani katika jimbo la Sudan magharibi la Darfur. Ripoti ilisisitiza makundi yanayohasimiana – yaani vikosi vya Serikali na waasi – bado yanaendelea kufuatilia suluhu ya mapigano kumaliza mvutano wao kwa sababu ya mzoroto katika utekelezaji wa Mapatano ya Amani ya Darfur.~

Ripoti ya KM kwa Baraza Kuu, juu ya hadhi ya wanawake wanaoajiriwa kwenye taasisi za UM, inasema maendeleo wastani, ya kuridhisha, yaliweza kupatikana kwenye kadhia hiyo. Ndani ya ripoti KM amebainisha kwamba utekelezaji wa lengo la kutekeleza usawa wa kijinsiya kwenye taasisi za UM unaendelea polepole sana na amependekeza kasi hiyo iharakishwe.

Misafara yenye kubeba misaada ya chakula ya Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) inaripotiwa kuelekea, kwa shida, kwenye yale maeneo yalioathirika na vurugu karibuni katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Vikosi vya Kanada ambavyo hutumiwa kuongoza misafara hiyo vinatazamiwa kumaliza kuhudumia shughuli hizo mwisho wa mwezi Oktoba, na vikosi vya Uholanzi vinatarajiwa kuendeleza shughuli hizo baadaye.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter