Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya Muungano wa Dini za Kimataifa kubuniwa rasmi Istanbul

Jumuiya ya Muungano wa Dini za Kimataifa kubuniwa rasmi Istanbul

Mkutano ulioandaliwa na Shirika la UM juu ya Mfuko wa Kudhibiti Idadi ya Watu (UNFPA) uliofanyika Istanbul, Uturuki kuzingatia mchango wa mashirika ya kidini katika kupambana na janga la UKIMWI .. na umaskini umemaliza mijadala yake ya siku mbili Ijumanne na kuafikiana kubuni jumuiya mpya itakayowakilisha dini zote kuu za ulimwengu, ikijumlisha Ukristo, Uislam, Uyahudi, pamoja na dini za Kihindu, Kibudha na Kisingasinga. Taasisi hii mpya itajulikana kwa jina la Jumuiya ya Mungano wa Dini za Kimataifa. ~