Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

M. Novak ahadharisha tabia karaha ya kufanya mateso kama desturi za kawaida

M. Novak ahadharisha tabia karaha ya kufanya mateso kama desturi za kawaida

Mkariri/Mtaalamu Maalumu Huru wa UM juu ya Mateso, Manfred Novak Alkhamisi alihutubia Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la UM ambapo alihadharisha kwamba katika uchunguzi wake wa kimataifa amegundua na kuthibitisha ya kuwa vitendo vya mateso vinaendelea kufanywa desturi za kawaida katika nchi nyingi za dunia.

Ilio baya zaidi, watu wenye ulemavu wa akili mara nyingi hutengwa na kuwekwa kwenye vyumba vya upweke magerezani, na hunymiwa huduma za afya, na hata hawapatiwi uangalizi wa wataalamu wa maradhi ya akili; na tumegundua hali ya watu waliopo vizuizini katika mataifa kadha wa kadha huwa wanasumbuliwa katika hali ya kutisha kabisa na kuhuzinisha sana, kwa mtazamo wa kiafya, watu ambao mara nyingi hawatunzwi kiafya, hupuuzwa na kusahauliwa kabisa na wenziwao waliopo nje. Mateso kama haya haifalii kimadili kuwepo hata kidogo katika ulimwengu wetu wa karne ya ishirini na moja.”