Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapatano ya serikali na wapinzani Usomali yaungwa mkono na UM

Mapatano ya serikali na wapinzani Usomali yaungwa mkono na UM

Ahmedou Ould Abdallah, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali ameyakaribisha mapatano ya karibuni baina ya Serikali ya Mpito Usomali na Jumuiya ya Ushirikiano wa makundi ya Upinzani ya ARS ya kusitisha mapigano, kuanzisha serikali ya muungano na pia vikosi vya taifa na kuondosha majeshi ya Ethiopia kutoka Usomali. Maafikiano haya yalitiwa sahihi Ijumapili kwenye taifa jirani la Djibouti katika tarehe 26 Oktoba (08).~