Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

KM amemteua Charles Petrie wa Ufaransa kushika wadhifa mpya wa Naibu Mjumbe Maalumu wa UM kwa Usomali. Petrie ana uzoefu wa miaka 18 katika kuhudumia sera za UM, pamoja na operesheni kadha wa kadha zinazohusu miradi ya maenedeleo. Vile vile Petrie alitumikia UM katika baadhi ya mizozo katika Afrika, ikijumlisha mgogoro wa Usomali. Hivi sasa Petrie ni Mshauri Maalumu wa Idara Inayohusika na Masuala ya Kisiasa (DPA) na pia UNDP.~

Ijumatano KM Ban Ki-moon alihutubia Kikao cha Pili cha Mkutano wa Kimataifa Kuzingatia Uhamaji na Maendeleo uliofanyika Manila, Phlippines. Kwenye hotuba alioiwasilisha mkutanoni KM alisema uhamaji unahitajia kutumiwa kama chombo cha kusaidia kuuvua umma wa kimataifa kutokana na mzozo wa uchumi uliokabili ulimwengu kwa sasa. Alitilia mkazo umuhimu wa kuwatekelezea wahamiaji haki zao, kitendo ambacho kikikamilishwa kitatuwezesha kuandaa, kwa mafanikio, mazingira yatakayoimarisha vizuri zaidi huduma za maendeleo.