31 Oktoba 2008
Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeeleza ya kuwa uhamisho wa mara kwa mara unadhuru sana kihali na kiakili watoto na wanawake – hali ambayo mara nyingi huchochea hatari ya kufumka maradhi ya kipindupindu na shurua, pamoja na ongezeko la utapiamlo mbaya miongoni mwa watoto.