Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Raisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Septemba atakuwa ni Mwakilishi wa Kudumu wa Burkina Faso ambaye atawasilisha ajenda ya mwezi ya shughuli za Baraza Ijumatano.

Modibo Tiemoko Traore, aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Vijijini na Serikali ya Mali amechukua madaraka ya Naibu Mkurugenzi Mkuu kwenye Idara ya Kilimo na Hifadhi ya Wanunuzi katika Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO). Traore alijiunga na FAO mwezi Machi 2008 kama Mwakilishi wa Ukanda wa Afrika baada ya kuongoza kwa miaka mitatu, kabla ya hapo, Taasisi ya Mataifa ya Afrika kwa Maliasili ya Wanyama.