Ripoti mpya ya UM haikuridhika na kasi ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia kimataifa

5 Septemba 2008

Ripoti mpya ya UM kuhusu maendeleo katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs)imewasilishwa rasmi wiki hii. ~~

Ripoti imewasilishwa kabla ya kuanza kikao maalumu cha hadhi ya juu kitakachokutana Makao Makuu ya UM, mjini New York, mnamo Septemba 25 (08), kikao ambacho kitaongozwa na KM Ban mwenyewe. Ripoti imegundua kwamba wahisani wa kimataifa wanatakiwa waongeze zaidi misaada yao rasmi ya maendeleo kwa kima cha dola bilioni 18 kila mwaka, kuanzia kipindi cha sasa hivi hadi 2010, pindi wamewania kihakika kuzitekeleza ahadi walizotoa 2000 za kupunguza umaskini kwa nusu, pamoja na kukomesha maradhi mengine ya kijamii, itakapofika 2015.

Sikiliza taarifa kamili kwenye idhaa ya mtandao.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter