Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Ijumatatu, Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji alihutubia kikao maalumu, cha mkutano wa mataifa wanachama 27 wa Umoja wa Ulaya (EU) uliofanyika Paris kuzingatia suala la hifadhi ya kisiasa kwa watu wanaotoka nchi za nje. Mkutano huu uliitishwa na Ufaransa, taifa ambalo kwa sasa ndio linaloongoza uraisi wa EU. Kwenye risala yake Guterres aliyasihi mataifa ya EU yaendelee na juhudi zao za kujenga mfumo mpya, wenye uwazi na unaoeleweka, kukabiliana na suala la hifadhi ya kisiasa na utakaotumiwa na wote.

Shirika la UM juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD) imetoa ripoti ya mwaka iliopewa mada isemayo Ripoti ya Msaada wa UNCTAD kwa Umma wa Falastina. Ndani ya ripoti UNCTAD ilionya ya kuwa uchumi unaojizoa zoa wa Falastina, ambao katika 2007 ulikua kwa kima cha sufuri taslimu, hautoweza kufufuliwa bila ya kuchangisha, kwa nguvu moja, zile sera zenye kuhusu udhibiti wa hazina za serikali, fedha, biashara na ajira. Ripoti ilisema ukomeshaji wa vikwazo vilivyoekewa maeneo ya Wafalastina na Israel pamoja na sera ya kuwanyima Wafalastina haki ya kutembea na kuhama ni miongoni mwa mambo ambayo ni lazima yakomeshwe kuweza kufufua uchumi kama inavyostahiki. Kadhalika UNCTAD ilipendekza ukuta wa vizuizi vya mtengano ubomolewe, na wahisani wa kimataifa wakithirishe misaada yao wakati Wafalastina wanachukua hatua za kulweta maguezi yanayofaa kwenye taasisi za utawala. UNCTAD ilitilia mkazo ulazima wa Utawala wa Falastina (PA) kuratibu, wenyewe, na kutekeleza sera za maendeleo ya uchumi na pia kuongoza namna ya kusimamia na ugawaji wa misaada ya maendeleo kwenye maeneo yao.