Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tathmini ya haki za wanawake Tanzania, kwa kulingana na CEDAW

Tathmini ya haki za wanawake Tanzania, kwa kulingana na CEDAW

Kamati ya UM ya Kuondosha Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW) kwenye kikao chake cha 41 mwaka huu ilisikiliza ripoti iliowakilishwa na Serikali ya Muungano wa Tanzania, kuhusu utekelezaji wa haki za wanawake katika taifa hilo. Kamati ya CEDAW, ni bodi la wataalamu liliobuniwa 1982, na linawakilishwa na wataalamuwa masuala ya haki za wanawake 23 kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Kila Kamati inapokutana kwenye vikao vya mwaka, hufanya mapitio ya ripoti za serikali za yale Maaifa yalioidhinisha na kuridhia Mkataba juu ya hatua zilizochukuliwa na zinazochukuliwa kuwatekelezea wanawake haki zao. Kwenye kikao cha mwaka huu Tanzania ilikuwa miongoni mwa Mataifa manane yaliowakilisha ripoti ya mapitio mbele ya Kamati ya CEDAW. Kikao hiki kilihudhuriwa, halkadhalika, na wajumbe waliowakilisha mashirika yasio ya kiserekali ya Tanzania. Redio ya UM ilifanya mahojiano na wajumbe wawili wa mashirika hayo ambao majina yao ni Jane Magigita, mwanasheria anayewakilisha kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake, pamoja na Nakazael Lukio Tenga, mwanasheria aliye wakili wa kujitegemea.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.