Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

~Shirika la UNAMID limeripoti ndege yao ya helikopta ilidungwa risasi Ijumapili katika eneo la Darfur Kaskazini na iliweza kutua salama na abiria ~12 pamoja na wafanyakazi 4 wa ndege, licha ya kuwa tangi la mafuta lilikuwa linavuja. UNAMID pia watumishi wake wawili walishambuliwa kwa risasi katika Darfur Magharibi na wahalifu wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa Janjaweed waliokuwa wamevaa unifomu za kijeshi amabao walionekana karioibu na Makao Makuu ya Sekta ya Magharibi ya Kijeshi.~

KM wa UM Ban Ki-moon na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Jean Ping wametangaza kumteua bia Azouz Ennifar wa Tunisia kuwa Naibu Mpatanishi wa Pamoja wa UM-UA kwa Darfur. Anatarajiwa kumsaidia Mpatanishi Mkuu wa UM-UA kwa Darfur, Djibril Yipene Bassole wa Burkina Faso. Ennifar ana uzoefu mkubwa katika dilpomasia, upatanishi na usimamizi wa ulinzi wa amani.

Haile Menkerios, Mjumbe wa KM kwa Zimbabwe Ijumatatu alihudhuria sherehe za utiaji sahihi wa mwafaka unaotarajiwa kusuluhisha mzozo wa kisiasa, taadhima iliofanyika kwenye mji wa Harare. Mchango wa UM kwenye juhudi za upatanishi ulitambuliwa kwenye hotuba za makundi yote yaliohusika na mgogoro wa Zimbabwe pamoja na risala ya Raisi Thabo Mbeki wa Afrika Kusini. Menkerios aliwasilisha pongezi za KM kwa Raisi Robert Mugabe, na viopngozi wa upinzani, Morgan Tsvangirai na Arthur Mutambara ambapo alitilia mkazo umuhimu wa kushirikiana kipamoja kuyatekeleza mapatano yao. Alisema UM ipo tayari kuunga mkono misaada ya faraja ya dharura ya muda mrefu pale serikali mpya itakapokamilisha orodha ya mahitaji ya kupewa umbele kuhudumiwa na jumuiya ya kimataifa nchini humo. Alisema UM upo tayari kusaidia katika maandalizi ya miradi ya maendeleo nchini Zimbabwe.