Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi 17 zakubali mapendekezo ya kudhibiti kisheria vitendo vya makampuni ya wanajeshi wa kukodi

Nchi 17 zakubali mapendekezo ya kudhibiti kisheria vitendo vya makampuni ya wanajeshi wa kukodi

Wataalamu kutoka nchi 17 waliokutana kwenye kikao maalumu kwenye mji wa Montreux, Uswiss kuanzia Ijumatatu (15/09/08), kuzingatia udhibiti bora wa shughuli za yale makampuni ya wanajeshi wa binafsi wanaohudumia usalama, hii leo wamepitisha warka maalumu uliosisitiza ya kuwa Serikali za Mataifa zina dhamana kuu ya kuhakikisha askari wakandarasi wa binafsi wanaokodiwa kushiriki kwenye maeneo ya uhasama na vita huwa wanafuata sheria za kiutu za kimataifa.

Nchi 17 zilizoshiriki kwenye mradi wa kudhibiti shughuli za makampuni yanayohudumia askari wa kukodi zilijumlisha Angola, Australia, Austria, Kanada, Uchina, Ufaransa, Ujerumani, Iraq, Poland, Sierra Leone, Afrika Kusini, Uswidin, Iswiss, Ukraine, Uingereza na Marekani.